SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imetoa gawio la shilingi Bilioni 11.7 kwa Serikali kwa mwaka 2025, likiwa ni ongezeko mara mbili walilotoa mwaka jana 2024 shilingi Bilioni 5.8.
Gawio hilo limetolewa leo Juni 10, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi husika, wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi TPDC Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mkurugenzi Mtendaji TPDC, CPA Mussa Makame.
Tuesday, June 10, 2025

Home
Unlabelled
TPDC YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 11.7 KWA SERIKALI
TPDC YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 11.7 KWA SERIKALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment