HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 20, 2025

TANZANIA KUANDAA JUKWAA LA KWANZA LA KITAIFA KUHUSU AKILI BANDIA (AI)

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TANZANIA inajiandaa kuwa mwenyeji wa jukwaa la kwanza la kitaifa kuhusu matumizi ya akili bandia (AI), litakalofanyika Julai 28 na 29, 2025 jijini Dar es Salaam, likitarajiwa kuwahusisha zaidi ya washiriki 500 kutoka sekta mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Tanzania, Dk Nkundwe Mwasaga, amesema jukwaa hilo ni la kihistoria kwa kuwa linakuja wakati ambapo teknolojia inabadilika kwa kasi, na mifumo inayotengenezwa na binadamu inaanza kuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi kama binadamu.

“Mabadiliko haya makubwa yanahitaji jukwaa la pamoja kwa watu kujadili kwa kina namna ya kuitumia AI kwa manufaa ya taifa, tukizingatia maadili, utawala bora wa taarifa na maendeleo jumuishi,” amesema Dkt. Mwasaga.

Aidha amesema katika jukwaa hilo, mada mbalimbali zitazungumzwa ikiwemo matumizi ya kawaida ya akili hunde, kuichambua akili hunde yenye uwezo wa kuchakata data na kutoa maudhui ambayo haikuwepo awali, kuangazia vitu vipya vinavyoibuka katika sekta ya akili hunde ikiwemo maadili.

Amesema kuwa sehemu nyingine zitakazoangaliwa ni namna itakavyoleta uwazi sambamba na kuleta Kampuni changa zilizojikita katika akili hunde kwa kuangalia changamoto zao na namna ya kuwasaidia.

Amesema kuwa kama nchi wanatarajia kupata ujuzi wa kutengeneza mifumo ya akili hunde au kuitumia, kupata taarifa na kujua namna ya kutengeneza sera ili matumizi ya akili hunde yawe salama, kubadilishana uzoefu, kupata fursa za kutumia bunifu zao kupata kazi katika taasisi mbalimbali.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad