Walio kaa kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Adolphina William na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza wakisaini mkataba wa makubaliano unaolenga kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo jumuishi kwa kuhakikisha wanawake na vijana wanapata fursa za kiuchumi, elimu, mikopo na msaada wa kitaalamu. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2025.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Adolphina William na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza wakionesha mkataba wa makubaliano unaolenga kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo kwa wanawake na Vijana. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2025.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Adolphina William na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza wakibadilishana mkataba wa makubaliano uliosainiwa jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2025.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana wajasiriamali wanaoshiriki katika minyororo ya thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini. Makubaliano haya ya miaka miwili yamesainiwa tarehe 17 Juni 2025 katika makao makuu ya TADB, yakihusisha viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili.
Mkataba huo, uliosainiwa leo Juni 18, 2025 na Dkt. Mwajuma Hamza, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC na Adolphina William, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, unalenga kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo jumuishi kwa kuhakikisha wanawake na vijana wanapata fursa za kiuchumi, elimu, mikopo na msaada wa kitaalamu.
Mambo Muhimu Yatakayotekelezwa katika mkataba huo wa Miaka miwili ni pamoja na Utafiti wa Kitaifa kubaini idadi na mahitaji ya wanawake wajasiriamali kwenye sekta husika ili kuweka mikakati sahihi ya maendeleo.
Mafunzo ya kujengea uwezo kulingana na matokeo ya tafiti, ili kukuza ujuzi na utayari wa kibiashara.
Uchambuzi wa fursa za kifedha na mikopo kwa wanawake na vijana wanaojishughulisha na minyororo ya thamani ya kilimo.
Upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia huduma maalum za kifedha kutoka TADB.
Msaada wa kitaalamu (Technical Assistance) kuhusu masuala ya fedha, masoko, matumizi ya teknolojia na uzingatiaji wa viwango vya kibiashara.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Adolphina William amesema makubaliano hayo yatawawezesha wanawake na vijana kwani ndiyo njia ya kuongeza tija kwenye kilimo.
"Ushirikiano huu unathibitisha dhamira ya TADB kutoa huduma za kifedha zenye kugusa moja kwa moja walengwa wetu.”
Kwa Upande wa Dkt. Mwajuma Hamza ameeleza kuwa makubaliano haya ni hatua kubwa katika kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika sekta ya kilimo.
“Kupitia ushirikiano huu na TADB, tunaamini tutaweza kuwafikia wanawake na vijana wengi zaidi na kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao zilizopo katika mnyororo wa dhamani wa kilimo, Uvuvi, Ufugaji pamoja na kilimo biashara.”
Makubaliano haya yataendelea hadi Mei 31, 2027, yakilenga si tu kuwa na matokeo ya haraka, bali pia kujenga msingi wa ushirikiano wa muda mrefu katika maendeleo jumuishi ya kijinsia na kiuchumi. Mpango huu unaendana na malengo ya taifa ya kukuza uchumi wa viwanda unaojumuisha makundi yote ya jamii.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Adolphina William akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2025 wakati wa kusaini mkataba wa makubaliono kwaajili ya kuwawezesha wanawake na Vijana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2025 wakati wa kusaini mkataba wa makubaliono kwaajili ya kuwawezesha wanawake na Vijana.
Matukio mbalimbali katika picha.
Picha ya Pamoja.
No comments:
Post a Comment