DAR ES SALAAM: TAASISI ya Miriam Odemba Foundation (MOF) inakusudia kufanya kampeni ya kuchangia damu, kutembelea wodi za wazazi na kutoa huduma zingine mbalimbali za afya tarehe 25 Julai mwaka huu, katika vituo vya afya jijini dar es salaam na maeneo ya jirani
Taarifa ya taasisi hiyo imeeleza kuwa lengo kuu ni kuwasaidia wamama waliojifungua, na walio katika hali ya uzazi, kuweza kujikimu na kujikwamua katika changamoto mbalimbali za uzazi zinazowakabili.
zoezi hili mahususi linalenga kuhamasisha watanzania katika kuwajali wanawake, wazazi na walezi nchini, huku pia vijana kwa zoezi zima la kuchangia damu kwa namna tofauti tofaufi nchini.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mwanziliishi wa taasisi hiyo, Miriam Odemba ameifafanua taarifa hiyo kuwa inagusa jamii nzima, na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki kwenye kampeni hiyo.
"Moyo wangu umejawa na upendo, na kuwajali vijana wa kike, na ndio maana tunathamini watoto pamoja na wazazi wao, ili kumjengea kijana wa kitanzania mazingira Mazuri ya mabinti wa kike
Taasisi hiyo pia inawakaribisha wadau wa afya na wengine mbalimbali watakaoguswa kwa namna tofauti tufauti katika kushiriki zoezi hilo
Miriam aliongezea kuwa kwa sasa taasisi inapokea Michango mbalimbali, misaada ya moja kwa moja, ya vifaa, huduma, na kadhalika
Miriam Odemba Foundation ni taasisi inayomilikiwa na Mwanamitindo nguli Mtanzania anayeishi Hispania, Paris, na Uswiss Miriam Odemba.
Aidha, taasisi yake imekuwa mstari wa mbele katika kumwezesha binti wa kike kutimiza malengo yake. wanafunzi wa kike taulo za hedhi, ujenzi wa vyoo vya shule mbalimbali na kusaidia wenye uhitaji.
No comments:
Post a Comment