CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetakiwa kuendelea kupanua wigo wa Wiki ya Utafiti na Ubunifu kwa kushirikisha washirika zaidi wa ndani na nje ya nchi, pamoja na kujumuisha tafiti bunifu kutoka sekta mbalimbali ili kuongeza manufaa ya kisayansi na kijamii.
Wito huo umetolewa leo Juni 11, 2025 na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Prof. Peter Msoffe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, wakati wa kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu katika UDSM.
Aidha amesema kuwa ikiwa tafiti zetu ambazo zinafanyika nchini zinaonekana na kueleweka na umma, itakuwa rahisi zaidi kuvutia wafadhili wa ndani na wa kimataifa na hatimaye kupata fursa nyingi zaidi za ushirikiano.
Amesema kuonesha kwa umma kazi za kitaaluma na matokeo ya utafiti kama mnavyofanya katika wiki hii ya ubunifu, ni hatua muhimu.
"Huu unaweza kuwa mwanzo mzuri wa kuishawishi Serikali na sekta binafsi kutambua na kuunga mkono jitihada za wanasayansi na wabunifu wetu, sambamba na kuboresha uhusiano baina ya vyuo vikuu na waajiri". Amesema
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Anangisye amesema UDSM itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na COSTECH na wadau wengine wa maendeleo ili kufanikisha upatikanaji wa ufadhili wa tafiti.
Prof. Anangisye ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa tafiti na ubunifu katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania na Taifa kwa ujumla kwa miaka mitano mfululizo wamekuwa wakitenga bajeti kwa kutegemea vyanzo vya ndani kwa ajili ya kufadhili tafiti na bunifu mbalimbali.
Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam-Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema kuwa katika maadhimisho haya wafanyakazi na wanafunzi toka vitengo mbalimbali vya kitaaluma vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamepata nafasi ya kuonesha na kuwasilisha kazi zao za utafiti.
Amesema kuwa jumla ya miradi ya utafiti na ubunifu iliyooneshwa na kuwasilishwa katika maadhimisho hayo ni ni 104. Hili ni ongezeko la kazi 27, toka 76 zilizoonyeshwa katika maadhimisho ya Tisa (2024).
"Kati ya kazi 104 za mwaka huu, kazi 65 (63%) ni za wafanyakazi na 39 (37%) ni za wanafunzi. Kazi hizi zimetathiminiwa na majaji kulingana na vigezo kategoria (categories) vilivyoainishwa. Kupitia tathmini husika, tumeweza kupata washindi kwenye hizo kategoria ambao wewe mgeni rasmi utawatunikia zawadi hivi punde". Amesema Prof. Boniface.
Amesema kwa ujumla, mahudhurio katika maadhimisho hayo yamekuwa makubwa kuliko ilivyotegemewa na ikilinganishwa na miaka iliyopita kwani waliongia na kuhudhuria makongamano na majadiliano mbalimbali walikuwa takribani washiriki 700, na kwa ujumla waliofika na kushuhudia maonesho na makongamano (kwa mujibu wa taarifa za kwenye mabanda) inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 1000.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Prof. Peter Msoffe akizungumza wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, wakati wa kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Prof. Peter Msoffe akizungumza wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, wakati wa kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam-Utafiti, Prof. Nelson Boniface akizungumza katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wa Utafiti na Ubunifu wakiwa katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Utafiti na Ubunifu wakiwa katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Utafiti na Ubunifu wakiwa katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa Utafiti na Ubunifu wakiwa katika hafla ya kufunga Maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu leo Juni 11, 2025 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
No comments:
Post a Comment