LIGI ya mabingwa ulaya (Uefa Champions League) imetamatika Kwa kumshuhudia PSG akitwaa taji hilo mbele ya Inter Milan na kuwa bingwa mpya wa michuano hiyo huku akiweka historia ya kubeba kombe hilo kubwa zaidi ulaya kwa mara ya kwanza. Ligi ya mabingwa imetumia mfumo mpya kwa mara ya kwanza. Chini ya kocha Luis Enrique, PSG ilibadili mfumo kutoka kwenye utegemezi wa majina makubwa ya wachezaji na kua timu yenye muunganiko wa vijana wadogo huku wachezaji muhimu wakiwa Vitinha, Desire Doue huku akichukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi na Ousmane Dembele aliyechukua tuzo ya mchezaji bora. Ushindi huu wa PSG unaipa nguvu Ligi ya Ufaransa (League One) ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikidharaulika na kuonakana kama ligi dhaifu (Farmers’ league). Wabashiri wengi wamepiga pesa na Meridianbet kwenye mchezo huu.
Goli bora la michuano hiyo limetoka kwa Lamine Yamal alilofunga dhidi ya Intermilan kwenye sare ya 3-3 hatua ya mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya michuano hiyo. Vinara wa ufungaji wakiwa Raphina wa Barcelona na Serhou Guirassy wa Borussia Dortmund waliofunga mabao 13 kila mmoja. Kikosi cha msimu kimeshuhudia majina mapya kama Golikipa Gianluigi Donnarumma (PSG), Walinzi, Achraf Hakimi (PSG), Marquinhos (PSG), Alessandro Bastoni (Inter), Nuno Mendes (PSG) Viungo, Vitinha (PSG), Declan Rice (Arsenal) na washambuliaji wakiwa Lamine Yamal (Barcelona), Désiré Doué (PSG), Ousmane Dembélé (PSG) pamoja na Raphinha (Barcelona).
Mechi ya ligi kuu Kenya, Gor Mahia dhidi ya AFC Leopards kukupatia maokoto leo. Suka jamvi lako hapa lakini pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, na mingine kibao.
Katika michuano ya kombe la Europa, Tottenham walitwaa ubingwa wao wa tatu huku wakivunja mwiko wa ukame wa mataji kwa klabu hiyo kutoka Uingereza. Tottenham walicheza fainali dhidi ya Manchester United na kuibuka kwa ushindi wa 1-0. Michuano hii pia ilishuhudia mabadiliko ya muundo wa uchezaji kwani zilishiriki timu 36 katika mfumo wa ligi badala ya ule wa makundi mawili uliozoeleka kwa miaka mingi. Jisajili na uweke bashiri zako kupitia Meridianbet kupata faida kubwa.
Goli la Yunus Akgün wa Galatasaray kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Tottenham limefanikiwa kuwa goli bora la mashindano hayo huku mlinzi wa kati wa Tottenham, Cristian Romero, akiibuka mchezaji bora huku kiungo wa Lyon Rayan Cherki akitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa kuipa timu yake magoli manne (04) na kutoa asaidizi wa magoli nane (08). Vinara wa ufungaji wakiwa ni Bruno Fernandes (Manchester United), Ayoub El Kaabi (Olympiacos) pamoja na Kasper Hogh (Bodø/Glimt). Waliofanikiwa kuunda kikosi bora cha michuano hiyo ni Golikipa Guglielmo Vicario (Tottenham), Walinzi, Pedro Porro (Tottenham), Cristian Romero (Tottenham), Robin Koch (Frankfurt), Fredrik André Bjørkan (Bodø/Glimt), Viungo, Patrick Berg (Bodø/Glimt), Bruno Fernandes (Manchester United), Casemiro (Manchester United) na safu ya ushambuliaji ni Rayan Cherki (Lyon), Dominic Solanke (Tottenham) pamoja na Nico Williams (Athletic Club).
Vilevile, UEFA Conference League imetamatika kwa Chelsea kutwaa ubingwa mbele ya Real Betis waliokua na msimu bora kwa kichapo cha mabao 4-1. Ushindi wa Chelsea unawapa rekodi ya kuwa timu pekee iliyofanikiwa kushinda mataji yote manne makubwa Ulaya. Isco (Real Betis) amefanikiwa mchezaji bora wa msimu huku Tobias Gulliksen (Djurgardens) akitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Kwa upande wa goli bora la mashindano, goli lake Fotis Ioannidis wa Panathinaikos dhidi ya Dinamo-Minsk limekua bora.
Kikosi cha msimu kimeundwa na Golikipa Filip Jørgensen (Chelsea), Walinzi, Youssouf Sabaly (Real Betis), Tosin Adarabioyo (Chelsea), Natan (Real Betis), Robin Gosens (Fiorentina), Viungo, Svit Sešlar (Celje), Isco (Real Betis), Enzo Fernández (Chelsea) pamoja na washambuliaji, Cole Palmer (Chelsea), Afimico Pululu (Jagiellonia) na Tokmac Nguen (Djurgården)
Michuano yote mitatu imeshuhudia mabadiliko ya kimuundo kutoka ule wa awali na kuingia rasmi kwenye mfumo wa timu 36 zinazocheza kwa mfumo wa ligi, jambo lililoongeza zaidi mvuto na ushindani katika michuano hii mikubwa zaidi barani ulaya. Kama hukuweka bashiri na Meridianbet, jisajili sasa michezo ipo mingi na pesa ni uhakika.
No comments:
Post a Comment