HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 24, 2025

RAIS DKT. SAMIA AWASILI MAPUTO NCHINI MSUMBIJI, KUWA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA JAMHURI YA MSUMBIJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi Maria Manuela Dos Santos Lucas mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo tarehe 24 Juni, 2025 Maputo, Jamhuri ya Msumbiji ambapo anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zitafanyika kesho katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi Maria Manuela Dos Santos Lucas mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo tarehe 24 Juni, 2025 Maputo, Jamhuri ya Msumbiji ambapo anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zitafanyika kesho katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad