HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 3, 2025

MIRADI YA BILIONI 44 KUPITIWA NA MWENGE WILAYA YA ILALA



MWENGE wa Uhuru leo umefika katika Wilaya ya Ilala amabpo mwenge huo unataraji kuzindua miradi Saba ya Maendeleo Wilaya ya Ilala, mkoani  yenye thamani ya sh bilioni 44 .5 na kukimbia km 82.6.  ukiwa pia umebeba ujumbe mzito wa uchaguzi wa Amani.

Akizungumza wakati anakabidhiwa Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alisema miradi hiyo ipo katika mitaa zaidi ya 18, Kata zaidi ya 18 za wilaya hiyo hivyo wananchi watapata fursa ya kuona mwenge na kushuhudia miradi ya maendeleo ikizinduliwa .

mara baada ya kukagua miradi ya Maendeleo Mwenge huo utakwenda kulala katika Viwanja vya Kampala Gongolamboto ambapo msanii maarufu Diamond Platnum atatumbuiza 








 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad