Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza wakati Uzinduzi wa Mfumo wa TANESCO wa Uwekezaji (TIMS)uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Isaac Chanji akitoa maelezo kuhusiana na umuhimu wa Mfumo TIMS wakati uzinduzi ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Lazaro Twange akitoa maelezo kuhusiana na safari ya kutengeneza mfumo wa TANESCO wa Uwekezaji (TIMS) wakati uzinduzi wa mfumo huo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Viongozi na Timu iliyotengeneza mfumo wa TIMS mara mara baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja viongozi pamoja na Wawekezaji katika miradi ya TANESCO.
*Aipongeza TANESCO kubuni mfumo wa kidijitali kwa wawekezaji
Na Mwandishi Wetu
NAIBU wa Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema kuwa kuweka mifumo ya kidijitali inaweka uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma na kuchochea kukua kwa uchumi.
Kapinga ameyasema hayo wakati alipomwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati Dkt.Doto Biteko wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Uwekezaji TANESCO (TIMS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa TANESCO kuzindua mfumo huo ni moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutaka mifumo ya serikali kusomana pamoja na mifumo mingine inayokwenda kuondoa usumbufu kwa wananchi wanapotaka huduma.
Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa kuna ufanisi katika sekta ya nishati kwa kuchangia pato la Taifa asilimia 14.4 kutoka asilimia Tano kwa miaka ya nyuma.
Aidha amesema kuwa mfumo wa TANESCO wa TIMS kutaongeza uwekezaji wa miradi ya umeme nchini kutokana wawekezaji wataingia katika mfumo na watajibiwa katika mfumo huo huo bila ya kufika ofisini na makaratasi.
Hata hivyo amewapongeza TANESCO kwa ubunifu wa mfumo huo uliokwenda kufanywa na watumishi ndani ya Shirika na kufanya Serikali kuokoa fedha katika kutengeneza mfumo huo wa kidijitali.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Lazaro Twange amesema kuwa mfumo huo utavutia wawekezaji wengi katika miradi ya umeme kutokana kuweka kila kitu ndani ya mfumo.
Amesema kuwa kinachofanyika kwa TANESCO kutekeleza maagizo ya Serikali juu ya kuwa na mifumo ya kidijitali katika kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma za uwekezaji.
Aidha amesema kuwa katika mifumo uwazi na uwajibikaji unaonekana na matokeo yake yanakua ya haraka kwenye utekelezaji.
Naibu Mkurugezi wa Mipango na Utafiti wa TANESCO Lenatha Ndege amesema kuwa wametengeneza mfumo wa kidijitali wa TIMS ili kuendana na kasi ya Serikali kuwa na miradi ya ubia na wawekezaji ambapo maombi yote yatafanyika ndani ya mfumo kwa watu wa ndani na nje ya nchi.
Lenatha amesema mfumo huo umetengenezwa kwa kutumia rasiliamali watu kutoka ndani ya Shirika kwa kufanikisha kwa weledi.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Isaac Chanji amesema kuwa mfumo huo kukamilika ndio adhima ya bodi katika shirika kwenda kisasa kwa kutumia mifumo ya kidijitali.
No comments:
Post a Comment