HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 28, 2025

MHASIBU SUA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SAME MASHARIKI

 

Kada wa Chama cha Mapinduzi, CPA (T) Ruth Hassani akisaini kitabu.
Kada wa Chama cha Mapinduzi, CPA (T) Ruth Hassani  ametia nia ya kuwania kuteuliwa na Chama chake kuwania Ubunge katika Jimbo la Same Mashariki, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Akiwa ameambatana na Mumewe Bw. Banyinga Majeshi, CPA Ruth ambaye ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Moprogoro alichukua fomu hiyo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same  na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya, Ndg.
Amos Kusakula leo Juni 29,2025.

Ruth amesema nia yake si kutafuta nafasi ya uongozi katika jimbo la Same Mashariki bali kuwasemea Wanasame Mashariki na kusaidiana nao kutatua kero mbalimbali zinazowakabili katika jimbo hilo na Same kwa ujumla akiangazia masuala ya elimu, huduma za Afya, Maji na nisshati safi. 

Katika kuwania uteuzi ndani ya Chama pia Mbunge anayemaliza muda wake Bi. Anne Kilango Malecela na Kada mwingine Bi. Miriam Mjema ni mingoni mwa wana CCM waliochukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea Ubge katika jimbo la Same Mashariki.

Jimbo la Same Mashariki lilianzishwa mnamo mwaka 1995 ambapo lilizaliwa kutoka Jimbo la Same hivyo ni moja ya majimbo mawili yanayoiunda Wilaya ya Same na ni moja ya majimbo tisa yanayounda mkoa wa Kilimanjaro.
Jimbo hilo linaundwa na Kata 14 ambapo Kata 5 ziko ukanda wa Tambarare na Kata 9 ziko ukanda wa milimani aidha lina vijiji 49 vyenye kaya 131350.

Wananchi wa Jimbo hilo kwa kiasi kikubwa wanajishughulisha na shughuli za kilimo cha Mpunga, Tangawizi, Mahindi, Maharagwe, Karanga, Ndizi, Kahawa, matunda na miti kwa ajili ya mbao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad