Katibu wa Chemba ya Migodi Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema mpango huo wa GGML umepunguza uhaba wa wahandisi na wataalamu wa fani mbalimbali kwenye sekta ya madini. Mkuu wa raslimali watu mafunzo na ujuzi wa Chama cha Waajiri Tanzania, Albert Rukeisa ameipongeza GGML kwa kulipa kipaumbele suala la usawa wa kijinsia kwenye mpango wa mafunzo kwa vitendo.
Albert amekiri GGML ni mdau muhimu katika kuendeleza taaluma ya usalama mahala pa kazi, kwa kulingana na mkataba wa ajira na mazingira ili kuzalisha kizazi chenye tija. Amesema vyama vya waajiri wote vimeingia makubaliano ya kuendeleza ujuzi na maarifa kazini, na tayari wameunda mabalaza ya ujuzi kwa kuanza na sekta ya madini ili kufikia adhima ya uwezeshaji vijana.
Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashimu Komba amesema mpango wa uwezeshaji ujuzi na maarifa ni matokeo chanya ya sera rafiki zilizowekwa na serikali kwa wawekezaji kufanya kazi kwa manufaa ya jamii nzima. "Uwepo wa uwekezaji huu mkubwa katika taifa letu unaruhusu teknolojia kuingia pamoja na kuhamisha ujuzi na maarifa kutoka mataifa makubwa na kurithishwa kwa watanzania", amesema.
Mmoja ya wahitimu 47 walionufaika na mpango huo mwaka 2025, Grace John amekiri mpango wa GGML utaimarisha taaluma zao na kuwawezesha kuingia kwenye soko la ushindani katika fani ya uhandisi.
No comments:
Post a Comment