Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu imezindua mfumo mpya wa kisasa wa ramani ya maeneo hatarishi, Tanzania Climate Vulnerability System (TVCVS), unaolenga kubaini mapema maeneo yanayokumbwa na majanga na kusaidia kupunguza athari kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akifungua mafunzo ya mfumo huo tarehe 16 Juni, 2025 katika ukumbi wa Kings Way Hotel, Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Brig. Jen. Hosea Ndagala, alisema mfumo huo utasaidia kufuatilia kwa karibu mabadiliko ya hali ya hewa na kutoa taarifa kwa wakati kwa sekta mbalimbali zilizo hatarini.
Mfumo huo unasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini -TMA, na taasisi nyingine, ukifadhiliwa na IMF na kuendelezwa na Global Center on Adaptation kwa usaidizi wa Masae Analytics.
“Mfumo huu ni sehemu ya juhudi za kitaifa na kimataifa za tahadhari ya mapema. Utasaidia kulinda maisha, mali, na kusaidia mipango bora ya maendeleo,” alisema Brig. Jen. Ndagala.
Washiriki kutoka sekta mbalimbali wamehimizwa kutumia mafunzo hayo kwa vitendo katika kupanga na kutekeleza miradi yao kwa kuzingatia athari za mabadiliko ya tabianchi.




No comments:
Post a Comment