HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 28, 2025

KULWA BITEKO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KATORO

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kulwa Biteko, amevuta fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo jipya la Katoro, lililoko Wilaya ya Geita. 

Hii ni mara ya kwanza kwa jimbo hilo kushiriki uchaguzi tangu kuanzishwa kwake mwaka huu, na Biteko amekuwa kada wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu, ambapo alitinga katika ofisi za CCM Wilaya ya Geita majira ya saa 8:20 asubuhi. 

Hatua ya Biteko imekuja mara baada ya CCM kutangaza rasmi kuwa watia nia wanaweza kuanza kuchukua fomu kuanzia Juni 27, 2025, fomu hizo ni kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Biteko alijaribu bahati yake kwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Busanda, ambapo aliongoza kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata kura 665, lakini hakuteuliwa kuwa mgombea rasmi wa chama katika jimbo hilo.

Kwa sasa, Biteko anaonekana kurejea tena kisiasa kwa nguvu mpya kupitia Jimbo la Katoro, akilenga kupata ridhaa ya chama na baadaye ya wananchi wa eneo hilo jipya.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad