Aidha, amesema vijana ni nguzo muhimu katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa, hivyo amewahimiza kuendelea kudumisha Amani, Mshikamano na kuwa na umoja.
Katibu Mkuu Fatma Hamad Rajab amesema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea, kukagua na kuzindua mradi wa kikundi cha vijana cha Tellary Group ulipo Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam Juni 4, 2025. Kikundi hicho kinajishughulisha na utengenezaji wa mikanda ya Gypsum na kilifanikiwa kuwezesha mkopo na Halmashauri ya Kinondoni kiasi cha shilingi milioni 97 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi zimeendelea kuchukua hatua Madhubuti za kuwezesha vijana kiuchumi kwa lengo la kuwapa fursa za kujiajiri.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi amesema Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha uzalendo na mshikamano wa kitaifa na kupitia ujumbe wa mwaka huu watanzania wanakumbushwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
Katika Wilaya ya Kinondoni Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekagua na kuweka jiwe la msingi pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa uzambazaji maji wa Mbopo Chekanao uliopo Mabwepande, Barabara ya Mediteranian, ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia na gesi ya mafuta ya petroli Kioevu ambayo inatumiwa na mama lishe na Baba Lishe katika soko la Tandale na ujenzi wa jengo la wagonjwa zahanati ya Hananasif.
Viongozi wengine walioshiriki katika Mbio hizo ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhuru Yunus, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba na Mkurugenzi wa wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Hanifa Suleiman Hamza.










No comments:
Post a Comment