HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 12, 2025

GCLA YAWAPA HAMASA VIJANA KUCHANGAMKIA MASOMO YA SAYANSI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetoa zawadi kwa kuwatunuku vyeti wanafunzi wahitimu 48 na walimu 8 waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024 kwa kutambua bidii na kujituma kwao katika kusoma masomo hayo.

Zawadi hizo zimehusisha mshindi wa kwanza hadi wa tatu kwa wasichana na wavulana kwa kila somo kwa kidato cha sita na kidato cha nne.

Akizungumza leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama, amesema kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeendelea na utaratibu wa kila mwaka wa kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika masomo hayo kitaifa katika mitihani yao ya kidato cha sita na nne.

"Kwa kuwa wingi wa ufaulu katika masomo hayo, ni ufanisi mkubwa katika maendeleo ya watoto wenyewe, shule wanazotoka, wazazi pamoja na taifa katika kuhimili matokeo ya ukuaji wa sayansi na teknolojia". Amesema

Amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali zenye kuwezesha na kutoa msukumo kwa wanafunzi kupenda kusoma masomo sayansi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya baadaye kwa vijana kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, na mchango wake kwa maendeleo endelevu.

Aidha amesema kuwa Serikali imewapa nafasi sawa watoto wa kitanzania kupata elimu kwa kuondoa ada kwa elimu ya msingi na sekondari, kuajiri walimu wa sayansi, kuboresha maabara na maktaba za kujifunzia, kuweka miundombinu mbalimbali kama vile vifaa na mifumo ya TEHAMA pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa na madawati.

"Mheshimiwa Rais hakuwasahau wanafunzi wenye changamoto mbalimbali kwa kuwawekea miundombinu rafiki katika shule wanazosoma ili kuhakikisha hawabaki nyuma katika kujipatia elimu". Amesema.

Kwa upande wa sekta ya Afya, amesema kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu hasa katika ujenzi wa majengo yenye kukidhi mahitaji na ununuzi wa mitambo na vifaa mbalimbali vya kisasa ili kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya Afya.

Amesema kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali, ni mnufaika mkubwa pia wa masomo ya sayansi ikihitaji watalaam wa kemia, vinasaba vya binadamu, sayansi ya chakula, mazingira, tiba asili na watalaam wa mitambo ya uchunguzi wa kimaabara ambao wote kwa pamoja wanahitaji kujengwa kupitia masomo ya Kemia, Biolojia, Hisabati na Fizikia.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu wa kutoa zawadi mwaka 2007 hadi kufikia leo, Mamlaka itakuwa imetoa tuzo na zawadi kwa jumla ya wahitimu/wanafunzi 432 na walimu 56.

"Tangu kuanzishwa kwake utaratibu huu umepata mafanikio mengi ikiwemo kuongeza hamasa kwa wanafunzi na kuongeza nguvu kazi ya wataalam katika sekta ya afya na sekta nyinginezo zinazohitaji taaluma ya sayansi". Amesema Dkt. Mafumiko.

Amesema takwimu zinaonesha tangu kuanza kwa utaratibu huo zaidi ya asilimia sabini na tano (75%) ya wanafunzi wanaozawadiwa hususani kwa kidato cha sita wanajiunga vyuo vinavyotoa taaluma ya afya ikiwemo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Chuo Kikuu cha Afya Bugando, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Herburt Kairuki.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa zawadi kwa walimu waliwawezesha wanafunzi wahitimu kufanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Dkt. Nyambea alimuwakilisha Waziri wa Afya Jenista Mhagama kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya sayansi wakiwa kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora zaidi wa somo la Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati kidato cha nne 2023 na kidato cha sita 2024. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 12, 2025 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad