Mradi wa Ubunifu wa FUNGUO, ambao ni mradi wa kimkakati unaofadhiliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Jamhuri ya Finland, na Serikali ya Uingereza (FCDO), na kutekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Tanzania), umetangaza rasmi uzinduzi wa fursa mbili muhimu za ufadhili zenye lengo la kuibua uwezo wa wajasiriamali wa Tanzania na kuchochea ukuaji endelevu katika sekta mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Karina Dzialowska, Mkuu wa Idara ya Uchumi na Utawala wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, amesisitiza dhamira ya EU katika kukuza ukuaji jumuishi na ubunifu. “Kilichoanza kama mradi wa majaribio miaka minne iliyopita, sasa umekuwa mhimili mkuu wa mfumo wa Tanzania:
FUNGUO limekuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara changa kwa msaada wa kiufundi na ufadhili unaowasaidia kukua na kufikia fursa pana za kifedha.” Amesisitiza zaidi, “Ninatoa wito hususani kwa vijana wanawake wenye ndoto na uthubutu. Tunakusudia angalau asilimia 40 ya ruzuku hizi ziende kwa wanawake, lakini hili litatimia tu kama mtawasilisha maombi yenu.”
William Nambiza, Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini Tanzania, amesema, “Kupitia #GreenCatalyst na ushirikiano wake kupitia Mradi wa Kusimamia Uhifadhi wa Misitu, Matumizi Bora ya Ardhi na Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu (FORLAND), tumejikita katika kuzalisha ajira rafiki kwa utunzaji wa mazingira, kulinda rasilimali, na kukuza ubunifu wa ndani kwenye mnyororo wa thamani wa misitu.”

Amesisitiza uungaji mkono wa Finland kwa Biashara Ndogo, Ndogo Sana, na za Kati (MSMEs), kwa kuongezea kuwa, “Tunataka kuchochea ukuaji wa biashara bunifu katika mnyororo wa thamani wa misitu, na tunatoa wito kwa wajasiriamali wengi zaidi kuwasilisha maombi na kuchangamkia fursa hii kupitia mpango wa #GreenCatalyst.”
Akisisitiza zaidi, John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, ameelezea umuhimu wa fursa hizi akisema, “Hii ni safari ya kujenga kizazi cha biashara zinazotatua changamoto halisi na kuleta mabadiliko endelevu.” Amepongeza mafanikio ya mradi, ambapo zaidi ya ajira 5,000 zimezalishwa na zaidi ya TZS bilioni 15 za ufadhili wa nyongeza zimekusanywa, kufuatia uwekezaji wa TZS bilioni 5.2 kwenye biashara changa 61.
Fursa ya kwanza ni Mpango wa #GreenCatalyst, dirisha maalum la ufadhili chini ya FUNGUO linalolenga kusaidia Biashara Ndogo, Ndogo Sana, na za Kati (MSMEs) zilizo katika hatua za mwanzo au za ukuaji zinazofanya kazi katika mnyororo wa thamani wa misitu nchini Tanzania. Fursa hii inawalenga wajasiriamali wanaobuni bidhaa au huduma kama vile useremala wa kisasa, bidhaa za mianzi, vifungashio rafiki kwa mazingira, mkaa mbadala, kilimo rafiki kwa misitu, utalii wa ikolojia, na huduma za kidijitali za misitu.
Kipaumbele kinatolewa kwa biashara zilizopo au zinazohusiana na mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, na Lindi, mradi unawapa kipaumbele vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu. Biashara zitakazochaguliwa zitapata ufadhili wa kuanzia TZS milioni 10 mpaka TZS milioni 100, pamoja na usaidizi wa kiufundi, kukuza biashara, upatikanaji wa masoko, zana za kidijitali, na mafunzo ya ubunifu unaozingatia mabadiliko ya tabianchi. Mpango huu unatekelezwa kwa kushirikiana na mradi wa FORLAND unaoungwa mkono na Finland, na kuchangia moja kwa moja katika kutengeneza ajira na uendelevu katika uchumi wa kijani wa Tanzania.
Kwa kuongezea, FUNGUO imezindua Awamu ya Nne ya Kutuma Maombi ya Ufadhili, inayolenga biashara bunifu za Tanzania zilizo tayari kwa ukuaji na ambazo zimeshaanza kuingiza mapato, ambazo zinalenga kuleta mabadiliko chanya. Unazikaribisha biashara zinazoonyesha ubunifu na uwezo wa kuleta mchango muhimu katika maeneo kama vile mabadiliko ya tabianchi, ajira kwa vijana, mabadiliko ya kidijitali, na maisha endelevu. Biashara zitakazochaguliwa zitapokea ruzuku ya ufadhili (bila hisa), msaada wa kujiandaa kwa uwekezaji, fursa za ushauri wa kitaalamu, pamoja na kuonekana zaidi ndani ya mfumo wa ubunifu wa Tanzania.
Fursa zote mbili sasa zimefunguliwa rasmi, na waombaji wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti rasmi ya FUNGUO: www.funguo.org
Mpango wa Ubunifu wa FUNGUO unaendelea kutoa ufadhili wa kuchochea maendeleo, usaidizi wa kiufundi, na msaada wa mfumo wa ubunifu kwa Biashara Ndogo, Ndogo Sana, na za Kati (MSMEs) bunifu za Kitanzania. Tangu kuzinduliwa kwake, mpango huu umewezesha biashara 61 kukua, kuvutia wawekezaji, na kuchangia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa.

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Utawala wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Karina Dzialowska, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa kampuni bunifu changa, biashara ndogondogo na kati zinazojihusisha na mazao ya misitu, kupitia programu ya FUNGUO chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere na kulia ni Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini, William Nambiza.
Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa kampuni bunifu changa, biashara ndogondogo na kati zinazojihusisha na mazao ya misitu, kupitia programu ya FUNGUO chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uchumi na Utawala wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Karina Dzialowska na kushoto ni Mkurgenzi wa Mazao Hub, Bw. Geophrey Tenganamba, ambayo ni mojawapo ya kampuni nufaika za programu hiyo.

Meneja Mkuu wa Programu wa Anza, Bi. Dina Kikuli, mshirika katika utekelezaji wa mradi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa kampuni bunifu changa, biashara ndogondogo na kati zinazojihusisha na mazao ya misitu, kupitia programu ya FUNGUO chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere na kulia ni Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini, William Nambiza.
Akisisitiza zaidi, John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, ameelezea umuhimu wa fursa hizi akisema, “Hii ni safari ya kujenga kizazi cha biashara zinazotatua changamoto halisi na kuleta mabadiliko endelevu.” Amepongeza mafanikio ya mradi, ambapo zaidi ya ajira 5,000 zimezalishwa na zaidi ya TZS bilioni 15 za ufadhili wa nyongeza zimekusanywa, kufuatia uwekezaji wa TZS bilioni 5.2 kwenye biashara changa 61.
Fursa ya kwanza ni Mpango wa #GreenCatalyst, dirisha maalum la ufadhili chini ya FUNGUO linalolenga kusaidia Biashara Ndogo, Ndogo Sana, na za Kati (MSMEs) zilizo katika hatua za mwanzo au za ukuaji zinazofanya kazi katika mnyororo wa thamani wa misitu nchini Tanzania. Fursa hii inawalenga wajasiriamali wanaobuni bidhaa au huduma kama vile useremala wa kisasa, bidhaa za mianzi, vifungashio rafiki kwa mazingira, mkaa mbadala, kilimo rafiki kwa misitu, utalii wa ikolojia, na huduma za kidijitali za misitu.
Kipaumbele kinatolewa kwa biashara zilizopo au zinazohusiana na mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, na Lindi, mradi unawapa kipaumbele vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu. Biashara zitakazochaguliwa zitapata ufadhili wa kuanzia TZS milioni 10 mpaka TZS milioni 100, pamoja na usaidizi wa kiufundi, kukuza biashara, upatikanaji wa masoko, zana za kidijitali, na mafunzo ya ubunifu unaozingatia mabadiliko ya tabianchi. Mpango huu unatekelezwa kwa kushirikiana na mradi wa FORLAND unaoungwa mkono na Finland, na kuchangia moja kwa moja katika kutengeneza ajira na uendelevu katika uchumi wa kijani wa Tanzania.
Kwa kuongezea, FUNGUO imezindua Awamu ya Nne ya Kutuma Maombi ya Ufadhili, inayolenga biashara bunifu za Tanzania zilizo tayari kwa ukuaji na ambazo zimeshaanza kuingiza mapato, ambazo zinalenga kuleta mabadiliko chanya. Unazikaribisha biashara zinazoonyesha ubunifu na uwezo wa kuleta mchango muhimu katika maeneo kama vile mabadiliko ya tabianchi, ajira kwa vijana, mabadiliko ya kidijitali, na maisha endelevu. Biashara zitakazochaguliwa zitapokea ruzuku ya ufadhili (bila hisa), msaada wa kujiandaa kwa uwekezaji, fursa za ushauri wa kitaalamu, pamoja na kuonekana zaidi ndani ya mfumo wa ubunifu wa Tanzania.
Fursa zote mbili sasa zimefunguliwa rasmi, na waombaji wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti rasmi ya FUNGUO: www.funguo.org
Mpango wa Ubunifu wa FUNGUO unaendelea kutoa ufadhili wa kuchochea maendeleo, usaidizi wa kiufundi, na msaada wa mfumo wa ubunifu kwa Biashara Ndogo, Ndogo Sana, na za Kati (MSMEs) bunifu za Kitanzania. Tangu kuzinduliwa kwake, mpango huu umewezesha biashara 61 kukua, kuvutia wawekezaji, na kuchangia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa.

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Utawala wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Karina Dzialowska, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa kampuni bunifu changa, biashara ndogondogo na kati zinazojihusisha na mazao ya misitu, kupitia programu ya FUNGUO chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere na kulia ni Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini, William Nambiza.

Meneja Mkuu wa Programu wa Anza, Bi. Dina Kikuli, mshirika katika utekelezaji wa mradi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa mradi wa ufadhili wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa kampuni bunifu changa, biashara ndogondogo na kati zinazojihusisha na mazao ya misitu, kupitia programu ya FUNGUO chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere na kulia ni Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini, William Nambiza.
No comments:
Post a Comment