HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 6, 2025

DC KINONDONI AWATULIZA WANANCHI MBOPO MGOGORO WA ARIDHI,AWATAKA WAWE WATULIVU

Na Mwandishi Wetu


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Saad Mtambule amewaahidi wananchi wa eneo la Mbopo kufanya ziara yenye lengo la kusikiliza kero pamoja na kutatua mgogoro wa aridhi kati ya wananchi na DDC ambao ndio wenye eneo hilo.

Katika eneo hilo DDC baada ya kuona wananchi wamevamia eneo hilo waliamua kutoa maelekezo kwamba wote ambao wamevamia wanapaswa kulipa fedha Sh.3000 kwa kila swekwea mita moja ili wamiliki kihalali lakini wao wanaomba Mkuu wa Wilaya kuingilia kati kumaliza mgogoro huo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Mbopo na
kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya 500,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati wanatafuta ufumbuzi wa mgogoro ambao tayari serikalini.

“serikali haitamuonea mtu itatenda haki kwa kila mmoja,kwani kazi ya Serikali ni kuhakikisha mwananchi anaishi kwa amani bila kubughudhiwa.”Amesema huku akitumia nafasi kueleza kuwa DDC hawakufika katika mkutano huo kwasababu ya kuwa na majukumu mengine.

Katika hatua nyinyine Mkuu wa Wilaya Mtambule amewaomba wananchi kuchangamkia fursa ya maji kupitia mkopo wa maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwani Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumtua ndoo mama kichwani na kufafanua mkopo wa maji mwananchi atatakiwa kulipa kwa awamu ndani ya miezi sita.

Kwa upande wake Diwani wa Kata diwani wa kata ya Mabwepande Mjirina Obama amesema ni vema wananchi wa Mbopo kuwa watuvulivu kwani mgogoro wa aridhi katika eneo lao tayari unashughulikiwa.

Awali katika mkutano wananchi waliwasilisha malalamiko mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa zoezi la upimaji wa ardhi na madai ya ukiukwaji wa haki za wamiliki halali wa viwanja.

Wananchi wanadai DDC imekuwa ikivamia maeneo ya watu na kuyapima upya kwa upendeleo. Imeripotiwa kuwa maeneo ya watu yanafinywa na kugawiwa kwa wengine bila ridhaa ya wamiliki halali.

Pia wananchi wamelalamika kutoshirikishwa kwenye maamuzi yanayohusu umiliki wa ardhi yao huku wengine wakidai wamegundua viwanja vyao vimegawiwa au kuchukuliwa bila hata kuitwa kwenye vikao husika. Pia, wamesema baadhi ya washiriki katika vikao hivyo si wakazi halisi.

Nae Mwananchi wa Mtaa wa Mbopo, Magwi Itembe akutoa malalamiko yake ya  kununua eneo kwa Tsh  35 Mln tangu 2015 ila DDC wameliweka alama kulichukua bila kumshirikisha na tayali amejenga kwenye hivo viwanja aliomba aingizwe kwenye program ya kulipia Tsh 3000 kwa sqm na yupo tayare kulipia kiasi hicho cha Fedha.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Saad Mtambule akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo, Mh Salum Suleiman Lyeme akizungumza.

Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mabwepande, Haruna Taratibu akisikiza kero za maji wakati wa mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni Jiji Dar es Salaam. Ambapo amewaomba wananchi kuchangamkia fursa ya maji kupitia mkopo wa maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)
Diwani wa Kata ya Mabwepande jijini Dar es Salaam, Muhajirina Kassim Obama.(kulia) akuwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo, Mh Salum Suleiman Lyeme .(katikati )
Mwananchi wa Mtaa wa Mbopo, Magwi Itembe akutoa malalamiko yake ya  kununua eneo kwa Tsh  35 Mln tangu 2015 ila DDC wameliweka alama kulichukua bila kumshirikisha na tayali amejenga kwenye hivo viwanja aliomba aingizwe kwenye program ya kulipia Tsh 3000 kwa sqm na yupo tayare kulipia kiasi hicho cha Fedha.




Mkutano ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad