HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 1, 2025

WATUMISHI WA TCAA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI

 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameungana na wafanyakazi wengine duniani kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ambayo kwa mwaka huu yameadhimishwa kitaifa katika Mkoa wa Singida, yakiongozwa na Mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki,” ikisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wafanyakazi katika mchakato wa uchaguzi kwa ajili ya mustakabali bora wa haki zao.

Katika kilele cha sherehe hizo, Mhe. Rais Dkt. Samia ametangaza habari njema kwa wafanyakazi wote nchini kwa kutangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 35, hatua inayolenga kuboresha maisha ya mfanyakazi na kutambua mchango wao katika ujenzi wa taifa.

Aidha, Maadhimisho ya Mei Mosi yameendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo Visiwani Zanzibar yaliongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, yakibeba kauli mbiu “Wafanyakazi tufanye kazi kwa bidii na nidhamu, tudai haki zetu kwa mujibu wa sheria na tushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa amani.”

Kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam, maadhimisho hayo yamefanyika kwa mafanikio makubwa yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Albert Chalamila.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya wakiimba Wimbo wa Mshikamano (Solidarity Forever) kwenye Maadhimisho ya Siku wa Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCAA Bi. Mtumwa Ameir alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kizimkazi, Unguja.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Zanzibar wakiwa kwenye maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kizimkazi, Unguja.
Gari lililobeba ujumbe wa TCAA katika maadhimisho ya Mei Mosi Kizimkazi  Kusini Unguja, Zanzibar. Gari hilo lilionyesha namna Wafanyakazi wa TCAA wanavyotoa huduma za Uongozaji ndege wakiwa kazini.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakipita mbele ya Jukwaa Kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad