Watumishi Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC),makao makuu na Kampasi ya Dar es Salaam
wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ ambayo kimkoa yamefanyika katika wilaya ya Kinondoni kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila ambapo amesisitiza kuwa wafanyakazi wanaposherehekea siku hii tutambue kwamba wao ndio wamebeba taswira ya serikali kwani mfanyakazi mmoja tu anaweza kusababisha serikali ichukiwe au ipendwe, hivyo wafanyakazi wote tuendelee kufanya kazi kwa uaminifu na imani kwani serikali inatujali na kutupenda.
Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 yalikuwa na kauli mbiu isemayo ‘Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’.
Baadhi Watumishi Chuo Cha Utumishi wa Umma wakipita mbele ya Jukwaa kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment