HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 6, 2025

Wananchi wampongeza Diwani Kata ya Kivukoni utekelezaji wa miradi

 

WANANCHI wa Kata ya Kivukoni, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, wamempongeza Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choghule kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hususan miundombinu ya barabara.

Wamesema, tangu aingie madarakani, diwani huyo amemaliza kero zilizo wasumbua kwa muda mrefu ukiwemo ujenzi wa Barabara za Sea View na Kimara.

Hayo yameelezwa na wananchi hao katika ziara ya diwani huyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mtaa wa Seaview, jana.

Mkazi wa mtaa huo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kapteni mstaafu John Chiligati, alimshukuru Diwani Choghule kwa ujenzi wa Barabara ya Sea View ambayo kwa kipindi kirefu ilikuwa kero kutokana na kuharibika vibaya.

“Kwakweli tunakushukuru kwa ujenzi wa barabara hii. Kulikuwa na madimbwi mengi hadi mbele ya nyumba za viongozi wa kubwa wan chi. Pia tufikishie salaam kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru sana,”alisema Chiligati.

Mkazi wa Mtaa wa Kimara , Multuzar gangji, alisema ujenzi wa Barabara ya Kimara kwa kiwango cha lami umekuwa suluhisho ya changamoto ya muda mrefu wa barabara hiyo .

“Kwa kweli tunakushukuru na tunaishukuru serikali kwa kutujengea barabara hii. Ilikuwa ni changamoto kubwa kutokana na ubovu . Changamoto iliyopo ni kuanguka kwa nguzo za simu na kusababisha nyaya kutawanyika barabarani. Tunaomba wahusika waondoe kero hii,”alisema Gangji.

Hata hivyo wananchi wa eneo hilo wamwomba Diwani Choghule, kushughulikia suala la ufinyu wa mitaro ambayo inakuwa kero kubwa hasa mvua inaponyesha.

Kwa upande wake Diwani Choghule, alimshukuru Rais Dk. Samia, CCM na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam , kwa utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba Sea View ya sasa saiyo kama ya wali.

“Barabara zimejengwa kwa kiwango cha lami. Mitaro hii itajengwa vizuri na kero itamalizika. Yote hii ni kazi ya Rais Dk. Samia,”alisema Choghule.

Katika ziara hiyo, Chighule alitembelea Kituo cha Mikutano cha Protea Hotel na Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaz Ocean Peal ambapo kesho ataendelea na ziara yake katika Soko Kuu la Kimataifa la Samaki Feri.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad