WADAU mbalimbali wa tasnia ya kutengeneza nishati safi za kupikia nchini wameshauriwa wanapokuwa kwenye mchakato wa kutengeneza nishati hizo kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kupata viwango vya kutengeneza nishati hizo.
Wito huo ulitolewa na Afisa Viwango wa TBS, Mhandisi Mohamed Kaila, wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika kongamano la siku tatu la nishati safi ya kupikia kwa nchi za Afrika Mashariki lililofanyika jijini Arusha wiki hii.
Alisema TBS ina maabara na vifaa vya kupima vifaa vya nishati safi za kupikia, hivyo jukumu lao ni kuhakikisha vifaa vyote vinavyoingia kutoka nje na vinavyozalishwa nchini vinakuwa vinakidhi viwango vya nishati safi ya kupikia, kwani shirika hilo lina wataalam wa kutosha na kila siku wanapima vifaa hivyo .
Aidha, alisema TBS inathibitisha ubora kwa wazalishaji wa ndani wanaozalisha bidhaa za nishati safi za kupikia na kwamba wakishamthibitisha anakuwa amepata leseni ya ubora kuwa anaweza kuuza ndani na nje ya nchi bila tatizo lolote.
"Kwa hiyo tunatoa wito kwa wazalishaji wa ndani wanaozalisha nishati safi za kupikia na wale wanaoagiza kutoka nje ya nchi kufika TBS ili kuhudumiwa katika suala zima la viwango vya nishati safi pamoja na uthibati," alisema Kaila na kuongeza;
"Kwa hiyo nishati safi ya kupikia bila TBS kutakuwa hakuna nishati safi ya kupikia nchi hii, kwa hiyo tunawashauri wadau wakati wakiwa kwenye tasinia nzima ya nishati safi ya kupikia kukaa na sisi kupata huduma zao za kutengeneza viwango .
Alisema TBS ndiyo wenye jukumu mama la kutengeneza viwango ili kuhakikisha nishati safi ya kupikia inakuwa kweli nishati safi ya kupikia.
Alisema katika kutekeleza jukumu lao hilo kuna vitu vya msingi wanaviangalia ambapo kitu cha kwanza ni usalama wa nishati safi za kupikia lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wnakuwa na uhakika kuwa vifaa hivyo viko salama.
Aidha, Kaila alisema pia wanaangalia suala la afya ili kumlinda mpishi , kwani wakati wa kupika kuna vitu vinaweza vikatokea kama moshi endapo nishati inayotumika si safi.
"Kwa hiyo kwetu sisi ili kufika kwenye nishati safi ya kupikia TBS tunaangalia suala hilo kwa umakini sana ili kulinda mtumiaji wa hiyo nishati," alisema Kaila.
Alitaja jambo lingine kuwa ni kuhakikisha wanatunza mazingira, hivyo wakati wa kutengeneza viwango vya hizo nishati, TBS wanahakikisha mazingira yanatuzwa..
Kwa mujibu wa Kaila jambo lingine wanaloangalia TBS ni uimara, kwani hawataki mtu anunue jiko leo baada ya miezi mitatu liwe limeharibika.
Pia Kaila, alisema jambo lingine wanaloangalia ni ufanisi wa nishati safi za kupikia ukoje, hivyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara , Wizara ya Nishati pamoja na wadau wa kitaifa na nje kama UNDP wameshirikiana kuweka viwango ili kupata nishati safi za kupikia .
Alisema kulingana na majukumu ya TBS kama hawatafanya vizuri kama wanavyoendelea kufanya vizuri hiyo nishati safi ya kupikia haitakuwa nishati ya kupikia.
Naye Afisa Afisa Viwango Spiradson Kagaba, alisema wakati tunaelekea kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia wanatakiwa kuhakikisha hakuna kinachoharibika,kwa maana ya kuhakikisha mtumiaji anakuwa salama na mazingira yanakuwa salama.
"Lakini pia mtumiaji aweze kupata kitu ambacho kiko kwa mujibu wa viwango," alisema Kagaba.
Alisema mojawapo ya matakwa ya viwango ni mzalishaji aseme ni kwa namna gani yale majiko yanafaa, anaweza kuja akasema ufanisi wake ni asilimia 90 kama TBS haijasimama ikamwambia yule mtu ni asilimia 80 ni rahisi sana huyo mtu kudanganya.
"Kwa hiyo sisi TBS tunaingia kuangalia yule mtu aliyetuambia ni la asilimia 80 ni asilimia 80 kweli anachosema mzalishaji," alisema.
Alifafanua kwamba TBS imefanya mambo mengi imeandaa viwango ili vitumike kuwalinda watu na kwamba wana viwango vya teknolojia zote kama ilivyotajwa kwenye mkakati.



No comments:
Post a Comment