HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 5, 2025

Uhuru wa Teknolojia Wafanikishwa, Vita Dhidi ya Malaria na Kilimo Salama Vyapata Nguvu Mpya

 



Tarehe 5 Mei 2025 Historia imeandikwa.
NI rasmi kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mmiliki wa teknolojia ya uzalishaji wa viuadudu (biolarvicides), viuatilifu hali (bio pesticides) na mbolea hai (bio fertilizer)

Shukrani za dhati kwa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuliwezesha hili kwa manufaa ya watanzania.

Sasa tunaweza kuongea kwa kujiamini kwamba ule mwisho wa ugonjwa wa malaria umefika. Sasa tunaweza kuongea kwa kujiamini kwamba tutazalisha mazao yetu pasina kutumia viuatifu na mbolea zenye sumu na zenye madhara kwa binadamu. Huu ni ushindi kwetu sote!

Hii ndio tafsiri sahihi ya Uhuru wa Nchi na Taifa, Utoshelevu wa kimaarifa, kiujuzi, kiubinifu, kiteknolojia, Ujamaa na Kujitegemea.
Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad