HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 22, 2025

TBS YAWAKUMBUSHA WANANCHI UMUHIMU WA KUJIRIDHISHA NA TAARIFA ZA BIDHAA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiridhisha na taarifa zilizo kwenye vifungashio vya bidhaa kabla ya kununua, likisema taarifa hizo ni sehemu muhimu ya uthibitisho wa ubora na usalama wa bidhaa husika.

Kupitia Meneja wa Ukaguzi na Utekelezaji wa Sheria, Nuru Mwasulama, TBS imeeleza kuwa moja ya majukumu yao makuu ni kuhakikisha bidhaa za chakula zinazingatia viwango vya ubora na usalama kwa kuzipima kwenye maabara na kuhakiki taarifa zinazowasilishwa kwenye vifungashio.

“Taarifa za kwenye vifungashio maana yake ni utambulisho wa bidhaa kwa mlaji. Zinakuambia bidhaa hiyo ni nini, inakupa maelekezo ya matumizi, uhakika wa ubora, usalama, na tarehe ya mwisho ya matumizi,” amesema Nuru.

Aidha, Baraka Mbajije, Afisa Mkaguzi Mwandamizi wa TBS, ametoa rai kwa wananchi kushiriki katika ulinzi wa afya zao kwa kutoa taarifa mara wanapokutana na bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi.

“Mtumiaji naye ana wajibu wa kuripoti bidhaa yoyote yenye dosari au iliyopita muda wa matumizi kabla mamlaka haijafika,” amesema Baraka.

TBS inatoa wito na kuendelea kuhamasisha wananchi kuwa na desturi ya kusoma taarifa za kwenye vifungashio kwani ulinzi wa afya zao unaanza na uelewa wa kile wanachonunua.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad