Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) amebainisha hayo leo tarehe 12 Mei 2025 wakati akiwasilisha bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.
Amesema kuwa lengo la mfuko huo itakuwa ni kuimarisha ubora wa kazi za watafiti na kukuza ushindani wa kitaaluma.
Pia amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa tuzo yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kwa utafiti utakaochapishwa katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa ili kuwahamasisha watafiti na wabunifu kuchapisha na kusambaza matokeo ya kazi zao na kuweza kutumika na wananchi.
Vilevile, Waziri Mkenda amesema kuwa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na ubunifu kikanda na kimataifa, Serikali itaendelea na mapitio ya Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (1996) ili kuwa na sera inayoakisi hali halisi na mahitaji ya sasa katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
Waziri Mkenda amesema, serikali itafanya tathmini ya Sera ya Taifa ya Utafiti na Maendeleo 2010, Sera ya Taifa ya Bioteknolojia 2010 na Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia 2013 ili kubaini hali halisi ya utekelezaji wa sera hizo.
Wabunifu na kazi za ubunifu ni chachu katika kuzalisha teknolojia mpya, kutatua changamoto za kijamii na kuchangia katika maendeleo ya nchi.






No comments:
Post a Comment