HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 30, 2025

SAKATA LA WANAFUNZI KUMGOBEA MWIJAKU LATUA KISUTU

 


HATIMAE wale, mwanafunzi watatu wanaodaiwa kumdhalilisha mwenzao ambae ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi, Dar es Salaam Magnificat Kimario wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Wanafunzi hao kwa sasa wapo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakisubiri kupandishwa kizimbani kutokana na video ya Aprili 20,2025 iliyozua mjadala mkubwa katika mitandao kijamii ikionesha wasichana wakigombana wakimuhusisha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwijaku.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi ya Aprili 24,2025 lilithibitisha kuwahoji wanafunzi hao ambao ni Mary Matogoro Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Ryner Mkwawili, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi, Dar es Salaam na Asha Juma Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam.

Pia, lilithibitisha kumuhoji Mwemba Burton Mwemba maarufu Mwijaku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad