HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 5, 2025

RWEBANGIRA ATEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA CHUNYA MKOANI MBEYA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira ametembelea na kukagua vituo vya kuandikishia wapiga Kura vilivyo katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa daftari unaojumuisha mikoa 15 nchini.

Mhe.Rwebangira ametembelea na kukagua kituo cha Ujenzi kilichopo katika Kata ya Itewe, Ofisi ya Kata Chokaa, Ofisi ya Mtendaji kata ya Matundasi, Ofisi ya Mtendaji Kata ya Makongolosi na Kituo cha Shule ya Sekondari Viwanja.

Aidha Mhe.Rwebangira ameendelea kutoa wito wa wananchi wa Mkoa wa Mbeya Kufika katika vituo vya kujiandikisha ili kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Pamoja na kuhakiki taarifa zkwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura ambalo limebandikwa katika kila kituo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad