HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 19, 2025

‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI WAGHUSHI RISITI

‎Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo kuhakikisha wanadhibiti waghushi risiti ambao wanaisababishia hasara serikali kwa kutokutoa risiti halali za EFD. 
‎Akizungumza ofisini kwake baada ya kupokea ugeni wa timu ya maafisa kutoka TRA Makao Makuu uliofika kwa ajili ya kuanza kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi kwa njia ya "Mlango kwa Mlango", Serukamba alisema kuwa ni muhimu kwa maofisa wa TRA kutoa elimu juu ya madhara ya kutoa risiti feki na adhabu zake pale mtu atakapobainika akifanya hivyo. 
‎Aidha, Mhe Serukamba amewahimiza wafanyabiashara wote mkoani Iringa kupokea elimu ya kodi kutoka kwa wataalamu wa TRA ili kuongeza uelewa juu ya masuala mbalimbali ya kodi.
‎Zoezi hilo linalenga pia  kuelimisha wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari, matumizi sahihi ya mashine za EFD, na kutoa risiti kwa kila mauzo. 
‎"Ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kutoa risiti halali kwa kila mauzo na kulipa kodi stahiki na hii itasaidia serikali kupata mapato ya kutekeleza miradi ya maendeleo,"amesema Serukamba.
Kwa upande wake Peter Jackson ambaye ni Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa,  ameeleza kuwa   kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na wafanyabiashara.
‎‎Amesema, hatua hiyo inalenga kubadilisha mtazamo wa wafanyabiashara juu ya mamlaka hiyo na kuongeza uwazi katika ulipaji kodi.

"Dhumuni letu hasa ni kuwashirikisha na kuwasaidia wateja wetu kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari. Pia tunataka kila mfanyabiashara aichukulie TRA kama mshirika wa maendeleo na sio adui wa biashara zao,” amesisitiza.
Kwa upande wao ‎Wafanyabiashara waliofikiwa na Elimu hiyo wameishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa uamuzi wa kutoa elimu ya mlipakodi mlango kwa mlango" maarufu kama door to door, wakisema kuwa hatua hiyo imewasaidia kupata uelewa mpana kuhusu masuala ya kodi na umuhimu wa kutumia mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFD).

Maafisa wanaofanya kampeni hiyo mkoani Iringa ‎wamefanikiwa kutembelea maduka ya wafanyabiashara na kutoa elimu ya kodi ikiwa ni pamoja na kupokea maoni, ushauri na kutatua changamoto za  wafanyabiashara hao.

Naye, Kelly Mnyawami ni mfanyabiashara eneo la Kihesa Manispaa ya Iringa  ambaye amesema, kutokana na elimu aliyoipata kupitia kampeni hiyo, hivi sasa atahakikisha analipa kodi kwa hiari na kwa wakati.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad