HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 11, 2025

RAIS MWINYI AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU CHARLES HILLAR

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Charles Hillary, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, tarehe 11 Mei 2025, jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. Mwinyi amefika nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu, Bi Sarah Mwakanjuki, pamoja na wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

Rais Dkt. Mwinyi amewataka wote walioguswa na msiba huo kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Marehemu Charles Hillary amefariki akiwa na umri wa miaka 66.

Rais Dkt. Mwinyi alimteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu tarehe 30 Desemba 2021, na baadaye akamteua tena kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 6 Februari 2023.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad