HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 9, 2025

RAIS DANIEL CHAPO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA KIKAZI

RAIS  wa Msumbiji Mheshimiwa Daniel Chapo tayari amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar Es Salaam ambapo akiwa Zanzibar atakua na ziara fupi ya kikazi

Akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hamza Hassan Juma pamoja na viongozi wengine akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nchini Tanzania Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo

Rais Chapo atakutana na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na kutembelea kituo cha Uvuvi cha Bahari kuu Fumba

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad