Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Mei 21, 2025 ametembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la awali unaoendelea katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar Katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani katika Jimbo la Uchaguzi la Pangani Mkoani Tanga.
Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.
Jaji Mwambegele aliwapongeza wananchi wa Pangani kwa namna walivyojitokeza kuboresha taarifa zao na kutazama daftari la awali lililobandikwa katika vituop mbalimbali walivyovitumia wakati wa uboreshaji wa daftari hapo awali.
Mkazi wa Mtaa wa Kimanga uliyopo Kata ya Kimanga, Wilayani Pangani, Mtwana Juma akionesha kadi yake baada ya Kuboresha
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akimkabidhi Kadi ya Mpiga Kura Mkazi wa Mtaa wa Kimanga uliyopo Kata ya Kimanga, Wilayani Pangani, Mtwana Juma leo Mei 21, 2025 wakati alipotembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la awali unaoendelea katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar Katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani katika Jimbo la Uchaguzi la Pangani Mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Pangani, Ndg. Charles Edward Fussi.
Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akisalimiana na wananchi wa Pangani waliojitokeza kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye kituo cha Soko la Samaki Pangadeco.
Jaji Mwambegele akimsikiliza Mwandikishaji Msaidizi wa Kituo cha Soko la Samaki Pangadeco Wilayani Pangani.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegelakiwa kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Pangani
No comments:
Post a Comment