HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 12, 2025

MKUTANO WA DHARURA WA MAKATIBU WAKUU WA USIMAMIZI WA MAAFA WA SADC WAFANYIKA DODOMA

Na. mwamdishi wetu

Mkutano wa dharura wa Makatibu Wakuu wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), umefanyika leo tarehe 12 Mei, 2025 kwa njia ya mtandao. 

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma, ukiwa na lengo la kujadili mikakati ya kukabiliana na maafa katika mikoa ya Kusini mwa Afrika.

Mkutano huu wa dharura umejumuisha Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa SADC, na umekuwa na mafanikio makubwa katika kubaini mbinu bora za usimamizi wa maafa, pamoja na kuboresha ushirikiano miongoni mwa nchi zinazokumbwa na maafa ya mara kwa mara.

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Eleuter Kiwhele, akiiongoza Tanzania katika mkutano huu, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kukabiliana na changamoto za maafa.

"Mkutano huu ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama wa SADC na kuhakikisha tunaongeza uwezo wetu katika kukabiliana na maafa na kuokoa maisha," alisema Bw. Kiwhele.

Aidha Bwana Kiwhele amesema, Kukabiliana na maafa ni jukumu letu sote, na ni muhimu kuwa na mikakati imara ili kuhakikisha kuwa tunajenga jamii zinazoweza kustahimili mabadiliko na changamoto za maafa.

Viongozi wa SADC wamezungumzia mikakati ya kuongeza ufanisi katika usimamizi wa maafa, pamoja na kugawana rasilimali na taarifa muhimu katika wakati wa dharura, hasa wakati wa majanga ya kiasili kama mafuriko, maporomoko ya ardhi na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huu umekuja wakati ambapo nchi nyingi za SADC zinakutana na changamoto kubwa za kimazingira, na umejikita katika kuhakikisha kuwa nchi wanachama zinakuwa na mifumo madhubuti ya usimamizi wa maafa ili kuokoa maisha ya watu na mali.

Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Usimamizi wa Maafa wa SADC umejikita katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa kwa nchi wanachama, ikiwa ni sehemu ya juhudi za SADC katika kujenga na kuimarisha ustahimilivu wa kiuchumi na kijamii dhidi ya maafa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad