HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 2, 2025

Mkurugenzi Zahara Michuzi atunukiwa cheti cha Mfanyakazi Hodari Mei Mosi Maswa

 




KATIKA shamrashamra za maadhimisho ya Siku  ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Comrade Kenani Kihongosi, alikabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Zahara Muhidin Michuzi, kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi.

Bi. Zahara alihamishiwa wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro, ambako pia  alihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita akifanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotambuliwa na wengi na kuacha alama zisizosahailika.

Tuzo hiyo imetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za viongozi na watendaji wanaoonyesha juhudi, kujituma, uzalendo wa kweli, ufanisi na uongozi thabiti katika utumishi wa umma, hasa katika, kusimamia miradi maendeleo, ukusanyaji wa mapato, kutatua kero za watumishi na wananchi kw ujumla sambamba na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.

Katika hotuba yake, Comrade Kihongosi aliwasihi watumishi wa umma kote mkoani Simiyu kuiga mfano wa Bi. Zahara kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama nzuri zisizofutika, uwajibikaji na moyo wa kizalendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad