HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 20, 2025

MHE. NYONGO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA NCHINI UBELIGIJI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo amewasili nchini Ubeligiji kuongoza ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Bajeti la Umoja wa Ulaya linalofanyika mjini Brussels nchini Ubeligiji kuanzia tarehe 20 hadi 21 Mei, 2025.

Tanzania imealikwa katika kongamano hili kama nchi pekee kutoka Afrika kushiriki katika kongamano hili kutokana na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Umoja wa Ulaya.

Katika kongamano hilo ujumbe wa Tanzania utatatoa maoni kuhusu mwelekeo wa vipaumbele vya bajeti ya EU kwa kipindi kijacho hususan katika maeneo yanayogusa maendeleo endelevu, uwekezaji, na ushirikiano wa kimaendeleo na nchi za Afrika.

Mbali na kushiriki katika kongamano hilo, Mhe. Nyongo ataongoza pia ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Afrika na Umoja wa Ulaya Mkutano huu muhimu unalenga kujadili masuala ikiwemo ulinzi na usalama, ustawi wa kiuchumi, , ushirikiano wa kimataifa na masuala ya uhamiaji.

Mhe. Nyongo amepokelewa na timu ya Serikali inayojumuisha: Mhe. Jestas Nyamanga, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Innocent Shiyo, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya,Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad