HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 14, 2025

MGODI WA UCHIMBAJI WA MADINI YA DHAHABU GEITA [GGML] KUSHIRIKIANA NA TAKUKURU KUTOA ELIMU YA RUSHWA MKOANI GEITA

Taasisi ya kupambana na Rushwa Mkoa wa Geita [TAKUKURU] imeandaa mpango wa kupambana na vitendo vya rushwa zinazojitokeza katika shughuli za maendeleo ya jamii zinazotekelezwa na Mgodi wa Geita Gold Mining Limited [GGML] kwa Mkoa wa Geita.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha iliyoandaliwa na Takukuru kwa kushirikiana na GGML Mjini Geita,Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita,Mohammed Gombati amesema swala la rushwa kwenye miradi ya kijamii sio la Takukuru pekee kwani wanatakiwa kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi pia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mining Limited [GGML],Duran Archery amesema rushwa ni tishio kubwa kwa ukuaji wa uchumi na utawala wa kidemokrasia duniani kote ambapo Mgodi huo kwa kushirikiana na Takukuru watafanya mikutano 28 ngazi ya vijiji na mitaa pamoja na vikundui vya uhamasishaji kupitia redio ili kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wa makundi yote katika jamii.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita,James Ruge amesema lengo la taasisi hiyo ni kudhibiti rushwa na kusisitiza kuwa taasisi hiyo itashirikiana na wadau mbalimbali.  

Kauli mbiu ya warsha ya mwaka huu ni 'Kuzuia Rusha ni Jukumu Langu la Lako - Tutimize wajibu wetu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad