HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 9, 2025

MARIAM ULEGA AHIMIZA WANANCHI MSANGA KUJIHAKIKI KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA



Na Mwandishi Wetu 

MJUMBE wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa jumuiya hiyo Mariam Ulega amewataka wananchi wa Msanga kujitokeza kupiga kura kwa sababu ni haki msingi kupiga kura.

Mariam ameyasema  hayo wakati  akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambapo amesisitiza ni vema wakahakiki majina yao katika  daftari la mpiga kura pindi uhakiki  awamu ya pili utakapoanza.

"Pia wale wananchi ambao wametimiza miaka 18 mwaka huu tunawahimiza kujiandikisha katika daftari la Kudumu la mpiga kura ili wakati wa uchaguzi mkuu utakapofika wapate haki yao kikatiba kichagua viongozi kwa maslahi ya Taifa letu."
Aidha amesema kuwa maendeleo yamefanyika chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya masuala maendeleo  yanaonekana hivyo anahitaji kuugwa mkono kwa kumpigia kura.

Mariam amesema kuwa  masuala ukatili wa watoto  yamekuwa ni mengi hivyo lazima wazazi  kuwa sehemu ya walinzi watoto hao huku akieleza hivi sasa hata wanaume nao wanapigwa na wake zao na huo nao ni ukatilii, hivyo ametoa rai kwa  wanawake waache kuwapiga waume zao na kuendelea na maisha ya amani.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad