HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 14, 2025

MANISPAA YA GEITA YAKUSANYA ZAIDI YA ASILIMIA 93

Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 18.05 sawa na asilimia 93.06 ya lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 19 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Myenzi amesema hayo katika kikao cha nne cha baraza la Madiwani kwa mwaka huu wa fedha na kueleza takwimu hizo ni hadi Aprili 30, 2025.

Muyenzi alisema tayari kiasi cha Shilingi Bilioni 7.2 ya mapato hayo ya ndani kimeshaelekezwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi ya elimu, afya, kilimo, miundombinu na biashara.

Amesema mbali na mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha pia Manispaa ya Geita imepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 2.63 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii.

Ameeleza pia wamepokea Shilingi Milioni 204 kati ya Shilingi Milioni 422 kutoka Mgodi wa Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu wa Geita (GGML) Pesa za uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR) kutekeleza miradi viporo ya mwaka 2018-2021.

Meya wa Manispaa ya Geita, Costantine Morandi amesema makadirio ya mapato ya ndani yamepanda kwa Shilingi Bilioni 11 ndani ya miaka mitano kutoka Shilingi Bilioni 5 mwaka 2020 hadi Shilingi Bilioni 19 mwaka 2025.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Michael Msuya amepongeza halmashauri kwa niaba ya chama na kukiri wazi kuwa viongozi waliopewa dhamana ndani ya manispaa wanawajibika.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad