HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 21, 2025

KUPITIA MRADI WA FEMA AILEADERS WABUNGE WABUNIFU NA MAKUNDI MENGINE WAPIGWA MSASA AKILI MNEMBA

 


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
KUPITIA Mradi wa FemAILeaders, Shirika la Women Political Leaders (WPL), GIZ Makao Makuu, GIZ Tanzania na Omuka imeandaa Mafunzo ya Akili Mnemba “Artificial Intelligence - AI” yaliyoanza Mei 19 hadi 20 mwaka 2025, Dar es Salaam yaliyolenga mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi wa mtandao,ubunifu na matumizi ya AI.


Mafunzo haya yaliwaleta pamoja Wabunge, Wabunifu na Makundi mengine kwa lengo la kuangazia ubunifu na matumizi ya AI, ulinzi wa kimtandao, utatuzi wa changamoto za AI na uhitaji wa kisera.


Delegation ya Bunge iliongozwa na Mhe Salome Makamba na kujumisha Mhe Prof Joyce Ndalichako, Mhe Esther Matiko, Mhe Ng’wasi Kamani na Makatibu wa Kamati za Bunge, Adv Ganjatuni Kilemile na Pius Katabazi.




Tanzania imeendelea kuongoza barani Afrika kwa Kuimarisha Uelewa na Ushawishi wa Wabunge Wanawake ili wawe Vinara wa AI hivyo kuchangia kwa Tanzania kunufaika na fursa zinazotokana na Akili Mnemba - AI. Tanzania imechaguliwa kuwa Mfano wa Kuigwa barani Afrika katika eneo hili.


Aidha, Mradi wa FemAILeaders umeweza kufanyika Tanzania kufuatia jitihada za Mhe Neema Lugangira (Mb) ambae pja ni Mwakilishi wa Afrika/Mjumbe Maalum wa Afrika wa Shirika la Women Political Leaders (WPL) hivyo ametumia nafasi hiyo kuileta fursa hii Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad