HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 31, 2025

KAMPUNI YA ZARA TANZANIA ADVENTURE YATOA VYETI VYA SHUKRANI KWA TAASISI MBALIMBALI NCHINI

 


KAMPUNI ya waongoza watalii nchini, ZARA Adventure, imetoa Vyeti Maalumu vya Shukrani kwa Taasisi, Kampuni na Mamlaka mbalimbali nchini, kama ishara ya kuthamini ushirikiano wao katika kuunga mkono utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, uongozi wa ZARA Adventure ulieleza kuwa vyeti hivyo ni sehemu ya kutambua mchango mkubwa unaotolewa na wadau hao katika maendeleo ya sekta ya utalii pamoja na mafanikio ya kampuni hiyo kwa ujumla.

Miongoni mwa taasisi zilizotunukiwa vyeti hivyo ni:
Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Utalii Dar es Salaam, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Bohari ya Dawa (MSD), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki ya NMB, Kituo cha Televisheni cha ITV, na Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASA).

ZARA Adventure imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha sekta ya utalii na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla.





Matukio katika picha ya uongozi wa ZARA Adveture wakiwakabidhi vyeti kutambua mchango wao.

1 comment:

  1. hawa jamaa wameshindikana katika kupandisha wageni mlima kilimanjaro , ni Kampuni bora sana wanaijua kazi yao , nimevutiwa sana na huduma zao na mwaka huy ,lazıma nipande tena .hongereni sana ZARA TOURS mpo vizuri

    ReplyDelete

Post Bottom Ad