Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Mohammad Ibrahim Sanya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma litakalofanyika Mei 11 hadi 13 katika Hoteli ya Golden Tulip Mjini Zanzibar.
ZANZIBAR
OFISI ya Msajili wa Hazina Zanzibar imeandaa jukwaa la kwanza la wakuu wa taasisi za uwekezaji wa umma litakalofanyika kwa siku tatu; Mei11-13, 2025 katika hoteli ya Golden Tulip Airport iliyopo visiwani humo.
Msajili wa Hazina Zanzibar Bw. Waheed Mohammad Ibrahim Sanya alisema Jumamosi, Mei 3, 2025 kuwa lengo kuu la jukwaa hilo ni kuwaunganisha wakuu wa taasisi kutoka taasisi mbalimbali za umma ili kujadili changamoto za pamoja, kubadilishana uzoefu, na kuanzisha mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji wa taasisi zao.
“Kupitia jukwaa hili, wakuu wa taasisi za umma wataweza kuimarisha ushirikiano, kubadilishana maarifa, na kuchochea ubunifu,” alisema huku akitabanaisha kuwa mgeni rasmi atakuwa Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Kaulimbiu ya Jukwa hilo ni “Uongozi Bunifu na Mashirikiano ni Muhimu ili kufikia Maendeleo Endelevu Zanzibar.”
No comments:
Post a Comment