HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 14, 2025

INEC, MKUU WA MKOA MOROGORO, WAJADILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI

 

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, baada ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro, yaliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mjini Morogoro leo Mei 14, 2025. Katikati ni Mjumbe wa INEC, Mhe. Balozi Omar Mapuri. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Balozi Omar Mapuri (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima wakati akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro leo Mei 14, 2025, kwa ajili ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima akizungumza na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Mapuri (Katikati) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima (kushoto), kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mjini Morogoro, leo Mei 14, 2025. 
 Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Mapuri (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, baada ya mazungumzo kati ya INEC na Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura, linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mkoani Morogoro, yaliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mjini Morogoro leo Mei 14, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima (wapili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Mapuri (watatu kulia), Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima (watatu kushoto), pamoja na Maafisa wa INEC na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, mjini Morogoro, leo Mei 14, 2025. Picha na INEC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad