Mkurugenzi wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi vya Excellent, Msaada Balula akizungumza wakati akifungua kambi ya uchunguzi na magonjwa mbalimbali na uchangiaji damu,Kibaha mkoani Pwani.
Mwanachi akifanyiwa uchunguzi wa sikio katika kambi ya Chuo cha Excellent Kibaha,mkoani Pwani.Wananchi wakiwa katika utaratibu wa kupata huduma za afya.
Wananchi na Wafanyakazi wa Chuo cha Excellent wakiwa wameshikana mikono kuonyesha umoja wao.
*Kimeweka mikakati ya kuzalisha rasimali watu wa kutoa huduma sekta ya afya
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
CHUO cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Excellent Kibaha mkoani Pwani kinaendesha kambi ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Mkoa huo ikiwa ni kurudisha mchango kwa jamii inayozunguka.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Kambi hiyo Mkurugenzi wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi vya Excellent Msaada Balula amesema kuwa umekuwa ni utaratibu wa katika kutoa huduma hizo katika maeneo ya vyuo kutokana kunauhitaji wananchi kupata huduma za afya kwa kuanzia vipimo pamoja na kila mwananchi kutambua afya yake mara baada ya kufanya uchunguzi.
Amesema kuwa katika kozi wanazozifundisha hakuna sababu ya kwenda kutoa huduma sehemu nyingine wakati mkoa husika wananchi wake wanaweza kufikiwa na huduma za afya.
Balula amesema kuwa kuwa wananchi wanahitaji huduma za afya ikiwemo uchunguzi wa magojwa mbalimbali ambapo wakati mwingine wanakosa fedha ya kufanya uchunguzi na kufanya kuziba nafasi ya wale wanaokosa fedha kupata huduma hizo bure.
Amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi ya kujenga kwa kujenga Hospitali,Vituo vya Afya ,Zahanati pamoja na Dispensari na kazi ya wadau imebaki kuwaanda rasilimali watu wa kwenda kuhudumia maeneo hayo.
Amesema Chuo cha Excellent kimeweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali watu ya sekta inapatikana ya kutosha katika vyuo vyao.
Amesema kuwa katika vyuo vya excellent wamekuwa na utaratibu wa kuchangia damu ambapo ambapo wameweza kuchangia damu chupa 1000 ambapo na kibaha wanatarajia kuchangia damu chupa 200.
Mwananchi wa Kibaha Halima Nakatona amesema wanashukuru Chuo cha Excellent kupeleka huduma za uchunguzi wa maginjwa mbalimbali kutokana na changamoto za uchumi wanashindwa kufanya uchunguzi afya zao.
Amesema kuwa kambi hiyo wanaomba kwa Chuo kuendelea kutoa mara kwa mara kwani msaada mkubwa kwao katika kujua afya kwani afya ndio msingi wa maendeleo.
Mratibu wa Huduma za Damu Salama Kibaha Mji Farida Chagula amesema kuwa amesema utaratibu wa chuo kuhamasisha uchangiaji wa damu ni jambo la kuigwa kutokana na uhitaji wa damu ni wa kila siku.
Amesema kuwa hakuna damu inayotengenezwa viwandani hivyo kila mwananchi anatakiwa kuguswa na suala la damu katika kuokoa maisha ya wengine
No comments:
Post a Comment