Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu CAG Ludovick Utouh ameishauri serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kutengeneza timu maalumu ya wataalamu itakayofanya uchambuzi yakinifu kwa Mashirika ya Umma na taasisi za serikali ambayo hayajiendeshi kwa faida na kuleta hasara kwa nchi.
"Kwa miaka mitatu mfululizo sasa serikali tumekua tunafanya vizuri sana katika makusanyo yetu ya mapato lakini utakuta kule kuzidisha mapato hakujatokana na bidii zetu za kuongeza mapato yetu ya ndani isipokuwa imekuwa na kukopa zaidi ya tulivyopanga CAG anatuambia kwamba kuna mabilioni yalikua yakusanywe na wahusika lakini hayajakusanywa hivyo zile pesa tunazozikusanya tuzisimamie na kuzitumia vizuri zaidi" amesema CAG Mstaafu Utouh.
Amesema kuwa timu hiyo maalumu itakayoundwa itapaswa kuaangalia kiini kinachosababisha hasara kwa mashirika hayo pia wafanye mapitio katika sheria zilizopo ikiwa pamoja na sheria ya manunuzi ya umma.
"Ipo haja ya kutengeneza sheria ya kuimarisha ofisi ya mkaguzi wa ndani na kuangalia utendaji wake ofisi hii bado changa kwani imeanzishwa mwaka 2012 ila ina umuhimu mkubwa, waweze kupata tarifa za utendaji wa serikali kabla ya ripoti ya CAG kutokelewa".
"Hali tuliyonayo sasa hivi fedha na rasilimali za nchi siyo za mtu bali ni pesa za wananchi, serikali imepewa mamlaka ya kukusanya hizo pesa kikatiba
"Hivi karibuni tumeona kwenye ripoti ya CAG serikali imefanya vizuri katika hesabu za serikali asilimia 95 za tasisi za serikali zimefanya vizuri.
Maafisa masuhuli wanafanya manunuzi bila kupata uhakiki kwa mwanasheria mkuu wa serikali, hivyo vinakua ni viashiria vya uhakika wa rushwa kuna haja ya watu wanaoteuliwa kwenye nafasi za uongozi wawe na uzalendo na kuthamini pesa za umma na kabla hujaitumia ifikirie kama pesa hiyo ingekuwa ya kwako je usingeithamini amesema CAG mstaafu Utouh.
CAG Mstaafu Utouh amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwamfipa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa Viongozi wa umma kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali nchini.
Baadhi ya Taasisi hizo ni Stamico, TTCL, TAMISEMI, Wizara ya Maji,TBA ,Youth Development, TARI ,TACAIDS,TBC,BIOTEC Kibaha Mji ,TANESCO, PCCBna Ocean Road.
Wakati huohuo Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Profesa Marcelina Chojoriga amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo washiriki hao 40 na kuwakumbusha majukumu yao ya kusimamia kwa weledi Mashirika ya umma na taasisi za serikali.
"Kiongozi ndiyo mbeba dira na maono hivyo viongozi lazima awe msimamizi mzuri na mwenye weledi ili aweze kuleta tija pia ni mbeba maonona dira ya kuwaendeleza wale anaowasimamia katika eneo lake".
"Wote tumeona na kusikia ripoti ya CAG lazima tukubaliane katika ushirikishwaji wa wananchi viongozi wawashirikishe katika mipango ya maendeleo kwani ni haki ya mwananchi kushirikishwa, sheria ya serikali ya mtaa inasema kila mwananchi mwenye umri wa mika 18 anatakiwa kushiriki katika mipango ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji wake hasa katika maendeleo na mipango ya serikali hivyo kila kiongozi atambue kuwajibika katika hilo".
No comments:
Post a Comment