Kuzuia uhalifu inasaidia Jeshi hilo kuweza kudhibiti madhara ambayo yanaweza kujitokeza lakini pia kusaidia kupunguza gharama za kuanza kufuatilia na muda pindi uhalifu utakapotokea.
Afisa wa Kamisheni ya Polisi Jamii,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Elisante Ulomi amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyawilimilwa iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Geita na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na pindi wanapohitajika kwenda mahakamani watoe ushirikiano.
Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi (SP) kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu Dodoma,Dkt. Ezekiel Kyogo amesema usalama ni uchumi,afya,amani na maendeleo wakati usalama utakapotoweka hakutakuwa na maelewano ambapo jamii ndiyo wawajibikaji wa kwanza kuweza kutunza tunu hiyo ya usalama kwa kushirikiana na jeshi hilo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi,Wilfred Willa kutoka Kitengo cha Dawakati la Jinsia na Watoto amewageukia wakina mama na kuwataka kuwachunguza mienendo ya watoto wao wakati wanaporejea nyumbani,wahakikishe wanawakagua watoto na kuwa karibu nao maana matukio mengi wanaobaini changamoto za watoto ni walimu baada ya kuona kiwango cha elimu cha mwanafunzi wake kinaanza kuporomoka na kuwapeleka hospitali na kukuta watoto hao wameharibikiwa muda mrefu.
Mwakilshi wa Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) Mihinzo Tumbo amesema Kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na jamii na wameshukuru muitikio wa wananchi ambao wanajitokeza kupata elimu hiyo ya usalama.
Mkutano huo ni mwendelezo wa Kampeni ya Siku 14 ya kufikisha elimu ya ulinzi shirikishi Mkoani Geita iliyoratibiwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
No comments:
Post a Comment