Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha RWAMGASA wameiomba serikali kuachia baadhi ya maeneo ya msitu wa hifadhi wa RWAMGASA kutokana na wakazi wa eneo hilo kuzunguzwa na shughuli za uchimbaji wa madini na kushindwa kulima na kufuga.
Wananchi hao wamesema mifugo yao imekosa maeneo ya malisho na kupelekea mifugo yao kukamatwa na kutozwa pesa na wamesema hakuna eneo lingine kwa ajili ya kulisha mifugo pamoja na kilimo.
Wananchi hao wametoa kero hiyo katika Mkutano wa wananchi,viongozi wa serikali na wa Chama cha Mapinduzi uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila.
Kwa upande wa serikali Mkuu wa wilaya ya Geita,Hashim Komba amesema msitu wa hifadhi ya Rwamgasa una ukubwa wa Hekta zaidi ya 28,000 na serikali imeshatengwa Hekta 10,000 kwa ajili ya kuwagawia wananchi kwa ajili ya kilimo na ufugaji wakati serikali ikiendelea kuweka utaratibu mzuri wa kuwagawia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila amemuagiza Mkuu wa wilaya Geita kuhakikisha anatatua kero zote zilizowasilishwa na Wananchi kwenye Mkutano huo kwa wakati.
No comments:
Post a Comment