Kutokana na mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na shughuli za kiuchumi kuanzia madini,kilimo,ufugaji na uvuvi wananchi wawe watulivu kutokana na miradi hiyo pindi utakapokamilika wawe tayari wameshajiandaa kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na haraka zaidi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholaus Kasendamila amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kayenze kata ya Kafita halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame amesema kwa kipindi cha miaka 4 serikali imeshaleta zaidi ya Shilingi BILIONI 4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwepo ya afya,elimu,utawala na tasaf.
Kingalame amesema kwa upande wa sekta ya maji wakazi wa wilaya hiyo kwa sasa wanapata maji kwa zaidi ya asilimia 77 na amesema wamekubaliana na RUWASA Wilaya ya Nyang’hwale kufikia mwezi Juni mwaka huu upatikanaji wa maji ufikie asilimia 85 kama serikali ilivyoelekeza.
Akizungumza baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Nicholaus Kasendamila kuruhusu maswali kutoka kwa wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Husna Toni akajibu moja ya hoja kuhusiana na utoaji wa elimu wa mikopo inayotolewa na halmashauri kwa makundi ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.‘Mikopo inatolewa kwa ajili ya biashara na wanaotakiwa kupata mikopo hiyo ni wale ambao wamejiunga kwenye vikundi na wanashughuli za biashara ambazo wanafanya kwa mfano ufugaji,ukulima n.k.’ amesema Husna
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Nichoalus Kasendamila anaendelea na ziara yake ya kuzungumza na Viongozi wa CCM wa wilaya na kuzungumza na wananchi hadi sasa wamefanya ziara wilaya ya Geita na Nyang’hwale.
No comments:
Post a Comment