HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 4, 2025

TOENI TAARIFA MAPEMA ZA UKATILI - ASP GRACE KAIJAGE

Umuhimu wa kutoa taarifa kwa wakati kwa waliofanyiwa ukatili wa kijinsia unasaidia kuzingatia afya na kupata matibabu mapema maana wananchi wengi wamekuwa na tabia wanachelewa kutoa taarifa na kuhatarisha afya zao. 


Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Geita,Mrakibu Msaidizi wa Polisi Grace Kaijage amesema ukatili wa kijinsia unaweza kutokana na kujeruhiwa mwili,kulawitiwa,kubakwa pindi unapotendewa ukatili wa aina yeyote ile wananchi,jamii,walengwa wa matukio hayo kuona umuhimu wa kutoa taarifa mapema. 



Kaimu Mwenyekiti (TPF-NET) Mkoa wa Geita, Kaijage amesema hayo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Geita iliyopo Mjini Geita kabla ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa wanafunzi hao. 

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya GEITA Lucy Beda amepongeza hatua ya Mtandao wa Polisi Wanawake wa Mkoa wa GEITA kufika katika shule ya sekondari na kutoa elimu na wajitahidi kufika hadi vijijini maana wengine wanaona kitendo cha ukatili ni matendo ya kawaida. 



Katika Mikoa mbalimbali nchini wamekuwa na matukio ya kusaidia au kutoa misaada mbalimbali katika jamii ikiwa ni kuelekea katika maadhimisho ya kilele ya Siku ya Mwanamke Duniani na kitaifa itafanyika Machi 8,2025 Mkoa wa Arusha na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.  




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad