HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 29, 2025

TLSB YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania  (TLSB )Dkt. Mboni Ruzegea amesema katika kipindi cha miaka minne (2021 - 2025) ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bodi imeweza kujenga na  kuboresha  Miundombinu, Ununuzi wa Vitabu ,Vifaa vya ujifunzaji pamoja na uanzishaji wa Maktaba Mtandao Jumuishi ya Kitaifa.


Hayo ameyasema Dkt. Mboni wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya Miaka Minne ya Bodi hiyo kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

 Dkt.Mboni  amesema  mafanikio ya bodi yametokana na serikali kutoa fedha  katika kujenga miundombinu ambapo imefanya kuwa kasi katika kutoa huduma za maktaba nchini.

 Amesema mafanikio mengine nj kufanya  Maboresho ya Sheria ya TLSB, Maandalizi ya Sera ya Taifa ya Huduma za Maktaba na Maendeleo ya Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS).

Aidha ameongeza kuwa, TLSB iko mbioni kuanzisha Maktaba za jamii ambazo zitaenda kuziba mwanya uliopo na kuwawezesha watu waishio maeneo ya pembezoni mwa miji na vijijini kunaufaika na huduma za Maktaba na kujiongezea maarifa na elimu.

Mkutano huo umehudhiriwa pia na Menejimenti ya TLSB, Wakutubi wa Mikoa na watumishi wengine wa TLSB, 

Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea akiwasilisha taarifa hiyo sambamba na picha mbalimbali katika Mkutano huo.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad