Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) alipokutana nao hivi karibuni, Ikulu ya Zanzibar waliofikika kumuelezea juu ya maendeleo na Mipango mikakati ya Jumuiya hiyo. Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania na Mkurugenzi Mwendeshaji ZSSF, Nassor Ameir (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt John Mduma, (watatu kushoto), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika na Tanzania, Meshach Bandawe (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu NHIF, Celestine Muganga pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu PSSSF, Rajabu Kinanda.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Saada Mkuya (aliyesimama) wakati akitoa utambulisho na maelezo ya awali ya ujumbe wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) iliyojumuisha Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini waliofika Ikulu ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi za Afrika (ASSA), Meshach Bandawe akiwasilisha taarifa fupi ya maendeleo na Mipango mikakati ya Jumuiya hizo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar, hivi karibuni.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo mafupi kwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment