Watoto wametakiwa kutokuoga wala kujifuta wanapofanyiwa ukatili wa kingono ili kutoondoa ushahidi unaoweza kusaidia kuwabaini wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Wito huo umetolewa na Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Geita wakati walipotembelea kituo cha watoto wnaoishi kwenye mazingira magumu cha Bright Light iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Geita na kutoa msaada wa vyakula,sabuni na taulo za kike kwa watoto 53.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la Polisi Wilaya ya Geita Christina Katana amesema, moja ya changamoto kubwa katika kesi za ukatili wa kijinsia ni watoto na waathirika wengine kuharibu ushahidi kwa kuoga au kujisafisha kabla ya kupimwa kitabibu.
Mkurugenzi wa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira cha Bright Ligh Methew Daniel amesema kituo kina watoto 53 wanaolelewa na kusomeshwa na kituo hicho.
Mtandao wa Polisi wanawake wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa siku ya maadhimisho ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini Arusha Machi 8,2025.
No comments:
Post a Comment