
Akizungumza na watafiti hao katika Hifadhi hiyo ya kipekee duniani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Stephano Msumi ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo muhimu ya kuwakutanisha watafiti wa Wizara hiyo na kutoka nchi Cuba kutembelea Hifadhi ya Serengeti ili kujionea changamoto hiyo kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wakudumu.
Aidha, amesema kuwa Hifadhi hiyo ni moja ya Hifadhi za Taifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia utalii hususani wa Wanyamapori hivyo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Wanyamapori wanapata malisho ya kutosha ni za kuungwa mkono.
Ameongeza kuwa, zipo juhudi zinazofanywa na wataalam kutoka katika Hifadhi hiyo za kupambana na mimea vamizi lakini bado hazijazaa matunda yaliyotarajiwa, hivyo uwepo wa watafiti hao kutoka Cuba na kuungana na watafiti wa Wizara hiyo ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya kuhakikisha malisho na usalama wa ikolojia ya Hifadhi hiyo ni endelevu.
Naye mtaalam mtambuzi wa mimea asili kutoka nchini Cuba, Dkt. Ramona Oviedo Prieto ametoa ushauri kwa wataalam wa ikolojia wa Hifadhi ya Taifa Serengeti kuchukua hatua za haraka za kulinda kingo za Mto Mara uliopo ndani ya Hifadhi hiyo kwa kurejeresha mimea ya asili iliyokuwepo pembezoni mwa Mto huo.
No comments:
Post a Comment